Skip to main content

Featured

Heavy responsibilities for elder aunt among the Logooli

With Seenge Fonesi. She is the elder grand daughter of Isagi and elder daughter of Amugasya. She is often present in functions involving the family of Amugasya. Pic taken on 18/4/2024. The elder sister soon becomes the elder aunt. It is this “seenge munene” (elder aunt) tag that she is tied to many cultural responsibilities – back home. To her marital family she may appear as any other woman, but she is not so in the eyes of her people. Marriage does not steal her away as it would happen with other daughters of the old man. To her, as days go and the old man and woman of the estate are dependents, she becomes increasingly present.  Her brothers also need her for almost all traditional markings. They are marrying, she needs to welcome the new wife. They are giving birth, she needs to come to midwife or “bless” the new born. They are paying dowry she needs to lead the women delegate. There is a conflict she needs to come for a hearing.  And many others. Traditions does not expect her to

Jinsi jina "Maragoli" lilianza

 

picha: Lango kuu la chuo cha sanaa cha South Maragoli

⨠Soma kwa lugha ya Lulogooli

Jamii yoyote duniani hupata jina lake kupitia njia mbili, kama sivyo wanajamii wapate jina hili kwa namna wanaovyojiita wenyewe, basi itakuwa inachangiwa na jamii jirani wanavyowaita. Na kwetu sisi jina la “Maragoli”, bila shaka ni majirani walivyotuita. Wakati mwingi jina hilo huwa na maana isiyotambulika vizuri na wenyeji. Wengine waweza kuendelea kulikubali jina hilo (k.m. “Bushman” Afrika Kusini) na wengine kulikataa (k. m. “Kitosh” Wabukusu). 

Asili ya jina “Maragoli” haijulikani vyema ingawa tunaweza kukisia jinsi jina hilo lilivyotokea. Kwa upande wa maana, au kwa ufahamu wake miongoni mwetu, jina “Maragoli” ni sawia na majina ya jamii kama Walogooli (wanajamii) na Evulogooli (sehemu wanakoishi). Inamaanisha kuwa jina “Maragoli” huchukua yote mawili; sehemu na watu.  

Kwa upande wa maumbo nao, pia ni jambo la dhahiri kuwa neno la “Maragoli” linapatikana kuwa na sehemu mbili: “ma” na “ragoli”. Katika sayansi ya lugha yaani isimu,  tunasema kwamba hivi vipashio vidogo vidogo katika neno moja vinaitwa mofimu (umoja wake pia unaitwa mofimu). Kwahiyo neno la “Maragoli” lina mofimu mbili: kiambishi-awali cha “ma-” na shina la nomino “-ragoli”. 

Hebu tuanzie na “-ragoli”. Dhana hii ya “ragoli” itajulikana vyema tukiangalia  jamii ambayo Mulogooli alifuatana nao. Jamii ambayo inasemekana kuwa karibu zaidi na Maragoli ni ya Kisii. Na katika lugha ya Kikisii, watu wanataja “Omoragori” kama kiongozi wa imani - kwa lugha ya Kiswahili Sanifu basi mlozi ukipenda. Kazi ya “Omoragori” ni kufuta bao yaani kupiga ramli na hata kufanya uganga. Sifa hizo zinaendana na zile za Mulogooli ambaye pia anayesemekana kuwa mtu wa imani ya kidini. 

Sasa tujaribu kukimulika kidogo kipashio cha “ma-”, ila tujue kwanza kuwa inawekezekana vyanzo vya kiambishi hiki labda ni vingi haswa kutoka Kimaragoli chenyewe au kutoka Kiswahili au kutoka Kijaluo. 

 Katika Lulogooli, lugha Kimarogoli yenyewe inavyotajwa, kiambishi cha “ma-” kina maana mbili kuu. Maana ya kwanza inajitokeza kwenye ngeli ya 6 {ma}. Ngeli hiyo haswa ni ya nomino kwa wingi. Mfano ni lisaanda – masaanda (kucha-makucha), livuyu - mavuyu (yai – mayai) na kadhalika. Maana kuu ya pili ni kwa nomino inayoelezea kitu cha zama,  kama mbegu au chakula, litapata jina lilogooli (mbegu ya kimaragoli) na malogooli (uwingi wa mbegu ya kimaragoli). Hii ikiwa na maana ya asili ya kitu hicho. 

Kwa upande wa ushawishi wa Kijaluo, historia kwa ufupi ni kwamba jamii ya Maragoli ilikuwa inafanya biashara na jamii ya Luo kwenye soko kuu la Kisumu, hata kabla ya mji wa Kisumu wa kisasa kuwepo. Inakisiwa kwamba jina la soko hili lilitokana na neno kusuma la lugha ya Kimaragoli ambalo linamaanisha “kupata vyakula na kurudi navyo nyumbani”. Wanabiashara watokao Maragoli huenda wakatangaza sana bidhaa zao kwa mkazo wa asili yao ya Maragoli, kama Maduuma Malogooli (mahindi ya Kilogooli), Mabwooni Malogooli (viazi vitamu vya Kilogooli) na kadhalika. Inawezekana matumizi haya mengi ya Malogooli yalipelekea hata wafanyabiashara hao wakaitwa Malogooli na wenzao sokoni. 

Hao wafanyabiashara Wajaluo, wakiwa jamii jirani, walijulikana kuita watu wa jamii mbalimbali za Wabantu _kwa majina ya “mar fulani fulani”. Hata siku ya leo kwa maneno ya Markakamega (wa kutoka Kakamega), Marabandu (wa kutoka sehemu za Uluyani) na kadhalika. Kwa muundo huu, mkiunganisha kitenzi-mizizi cha kuroga yaani -logola (au -lagula kwa sababu ya tofauti baina ya lahaja za viluyia) mtapata "Marlogola" (au "Marlagula). Hivyo, haingekuwa ajabu sana neno likabadili kuwa Maragoli kwa sababu ya matamshi tofauti tofauti enzi za zamani. 

Na si kwa biashara tu ambapo Waluo na Wamaragoli walipatana. Pia kwenye ukoo, wakajulikana sana kuitana “mashemeji” hadi hii leo. Lakini si sahihi kwamba hawajawahi kuwa na mvutano, inasemekana jina la kijiji cha Chulaimbo lina maana ya "rudi uluoni", pale Wamaragoli walipigana nao. Tukifuata mantiki hii, pia tukumbukwe hata Wajaluo huita vita “gore”, basi haukosekani uwezekano wa Wamaragoli waliotajwa “Margore” katika historia, kumaanisha wanavita. 

 Kwa Kiswahili, moja ya matumizi ya ma- ni kujulisha pahali.  Neno kama “makwao” au “makaazi”, tukiacha umbo la “-kwao” au “-kaazi” tubaki na umbo la “ma-” tujue hakika hii inamaanisha pahali.  Neno lingine kama “madachi” linatokana na "ma-" na "-dachi" na hapo “ma-” inamaanisha uwingi wa watu na “-dachi” kumaanisha The Dutch kwa Kiingereza ila wakati huo zamani “madachi” pia lilimaanisha Wajerumani. Neno “maragoli” basi lina maana ya sehemu, watu au zote kwa pamoja vivyo hivyo linavyotumika hivi sasa. Na ikiwa Kiswahili kilichangia pakubwa, basi chaweza kuwa sababu kuu ya kiambishi "ma-" cha pahali. Pamoja na kuwa lugha ya Kimaragoli ilijulikana kama "Ragoli" wakati wa uandishi wa kwanza na Friends Africa Mission, 1907 kutolewa.  Hii “ragoli” iliwezekana kuwekwa “ma” kwa sarufi ya Kiswahili kwa sababu Kiswahili ilitumika pakubwa kwa marejeo ya maandishi ya lugha za kibantu. 

Punde tu baada ya maandishi yaliyoamuliwa, basi haukupita muda mrefu pale jina la Maragoli likashika mizizi sana. Mfano ni sanduku la posta P.O. BOX 50300 Maragoli. Mfano mwingine ni milima ya Maragoli, iliyoitwa Maragoli Hills. Hata jamii yote ya Waluhya, kwa watu wa mbali kama Kuria wanaoishi na Wamaragoli waliohamia kule, husema Uluyani ni kwa Maragoli. 

Hata hivyo juhudi za kutambua ujio wa jina "Maragoli" zinahitajika.  Uchunguzi huo utatiliza mkazo jina Maragoli Cultural Festival, sherehe ambayo inaeziwa sana na Walogooli na hufanyika kila mwaka, Disemba 26. Ni ukweli sherehe hii ni ya "kuonyesha Ulogooli" kwa dunia asili na majivuno ya kijamii kama walivyofanya wanabiashara enzi za zama. Hivi sasa uonyeshaji ukiwa mafunzo na ustaarabu.  

Comments