Saniaga Sacco kuanza kirasmi mnamo 08/06/2019
Haiya basi. Mbiu ya mgambo imelia.
Kila mmoja wetu ajiandae. Shirika la Saniaga Sacco latarajiwa kuanza kazi kirasmi ifikapo Jumamosi Juni nane mwaka huu.
Kabla yake, maandalizi yatahitaji upya wa mtazamo tulio nao, msimamo imara na umarudufu wa jitihada zetu.
Nitawaomba tujiandae vilivyo kwa kuekeza. Kopo letu lishone. Tunao uwezo, tunazo nia. Kilicho kati yetu na timisho la maono ni juhudi tu. Nayo, tutatimiza.
Kinyozi wangu amenoa nyembe. Aniita. Tumalizanapo nitarudi nikiwa na imani kwamba nimejiweka katika hali nzuri ya kupata uungwaji mkono mkubwa kwa jitihada zetu za kuijenga nyumba ya Saniaga.
😁😁😁😎😎😎.
Asante.
Comments
Post a Comment