Mijadala ya shule za msingi - 2019

Maktaba ya S-CBO itahusisha shule 15 za msingi muhula huu wa pili kwenye mashindano ya mijadala yenye mada *Nyimbo za kale* . 

Muhula uliopita tulihusisha shule 8 zilizo karibu na maktaba ya Wangulu kwenye mashindano yaliyofana mno. Mada ilikuwa kwa kimombo; *application of mother-toungue as a guiding and counselling tool in primary schools*. Wanafunzi walioshiriki walipata fursa ya kujifunza uzuri wa lugha ya mama katika ujumla wa ukuzi bora wakiwa shuleni. 

Wanafunzi wanatarajiwa kufahamu vyema nyimbo za kale. Matumizi, maana, tofauti, ala, uigizaji wazo pia. Ufahamu huu utawasaidia kueleza pande zao za mijadala - ikiwa waunga mkono au wapinga mjadala. 

Saniaga ina jukumu kubwa la kutambua, kuhamasisha, kuhusisha, kuendeleza na kuhifadhi sajili asili ya jamii. Mijadala ni mojawapo ya njia za kutimiza malengo hayo. 

Tunakaribisha mawazo na usaidizi kwa kila anayehusika kufanikisha mada ya muhula huu. 

- Asante

Comments