Skip to main content

Featured

Luanda Reggae Defenders - what is your long term agenda?

Luanda Reggae Defenders is a now a popular movement with roots in Vihiga and border Siaya and Kakamega counties Attention is brought to the manner and conduct the movement has gained fame and followers, mainly the Youths. The movement capitalizes on funerals. With a poor culture of putting the dead to rest, the Reggae Defenders have taken it by storm and rebranded the infamous ‘Disco Matanga’ – disco at funeral. Reggae Defenders on move. Pic: Charles Rankings: Facebook They mobilize quickly on the day the dead will be discharged from the mortuary. They have this huge old school sound system that is over buzzing to no clear reggae song - that they hire a pickup to carry - and it has a young DJ mainly standing there than mixing anything. Often, against the rules, the casket is grabbed from a hearse vehicle and tied to a motorbike. There it will be swayed and jerk breaked between other motorbikes on the narrow roads. That, is, how a fellow soldier, often a young dead, is mourned. ...

Ukombozi tunaouhitaji

Sam wa Sundi: Haha, mjomba upo?

Lung'afa: sipo. Kuwepo kwangu ni fedheha humu duniani. Nimeasi uwepo wote uliopo.

Sam wa Sundi: Mazito mithili ya kaburi haswa

Lung'afa: ilhali wanaoyasoma wanasoma na ndimi tu, sio akili

Sam wa Sundi: Itakua vyema wakisoma na akili, huu ni mwanzo tu wa ukombozi wa tatu, ukombozi wa mawazo na hisia.

Lung'afa: Ukweli mwanangu. Butangi sasa haihitaji ukombozi wa kifalme wala rasilmali. Butangi yahitaji ubadilifu wa mawazo, uzoefu wa kutumia jicho la tatu, mambo ambayo kwa wengi ni hadithi.

Sam wa Sundi: Ni bayana sasa tunaelekea shimo la moto wa uoga ambalo limefunikwa na moshi wa amani. Ati tukitaka salama yetu, tuzingatie amani bila kuulizia haki. Wakati moshi utatuingia machoni na kukwama kwa mapafu, tutagutuka tukiwa jivu.

Lung'afa: Tumedanganywa tugadanganyika na mafunzo ya kikoloni ambayo yameanzia kwenye familia kuelekea shuleni. Wana hawafunzwi historia yao, wao ni wakuiga tu. Wazazi hawana la kuwasemesha, wao jicho tu bora mtoto avalishwe mavazi na ale pojo. Hayo yakitendeka kule mbele mkoloni azidi kuzindua na kufumbua ulimwengu kwa uongo wa teknolojia ambao utamupiku yuyu huyu kimwani kisichojua tofauti ya pengo na kicheko. Kawaone vile wamebebana vichwa toka huku hadi kule ukadhani wanaenda kuendekako. Giza!

Sam wa Sundi: Giza totoro. Giza kuu. Na ndio maana nimefika mwisho, na kuanza mwanzo wangu mpya, mwanzo wa kuleta majibu halisi, wala sio majibu ya kufikirika na kutamanika tu. Majibu ya kueleza na kuthibitisha kwamba kwa kweli mwafrika pia amekua na safari yake na bado yu mbioni kuafikia makubwa mengi.

Lung'afa: Tumo mbioni. Wengi watatupata njiani. La mno ni kutia kamba kiunoni yawe yaweje hakuna kugeuza kichwa kisogoni. Na mwanzo ni nafsi yako wewe mja mmoja.

Sam wa Sundi: Wengi ni nafsi moja iliyokwisha kuamua, hivyo ndivyo mimi natafsiri wengi katika shule yangu ya kimawazo. Wengi isimanishe halaiki iliyojaa sokoni, uwanjani, ukumbini wala barabarani. Lakini iwe ni nafsi moja ambayo imeamua kutembea njia ya kujivunia uhuru wa nafsi.

Lung'afa: Mbona niyaseme tema ilhali umeyawaza tayari? Wengi ni wewe, wachache ni yule asiye na uhakika na lengo lake humu duniani. Muchache ni yule anayepapasa vikoba miguuni mwake asije akahisi mkato wa baridi la umakinifu. Mimi najipa jina la Sisi, na atakayeuliza Sisi ni nani basi jibu kwake litakua Mimi Niliyeopo.

Sam wa Sundi: Nakuunga mkono. Na wengi wetu ndio utakua asubui njema, asubui ya matumaini. Na siku itakua ishara tosha kwamba binadamu hawezipinga wakati.

Lung'afa: Usoni kule mwanadamu huashiria ukombozi wake ni ishara tosha ikilinganishwa na mbwa aliye kwenye jabali lililoegemea dimbwi. Pale anapomuona ndege akamurukia ndipo mwisho wake. Binadamu hawezi jikomboa kwa kujiwazia na kujitungia siha kama ulivyodai hapo awali. Ukombozi wake umo mule alikotoka, pale mwanzo, ile dini aliyoanza nayo, kabla ajifahamu kuwa yeye ni binadamu, pale mawazo yake hayakuwa na tamaa wala uovu. Kule kuliko giza la nuru. Giza ambalo lilifadhahishwa na ujaji wa wageni. Kumbe yao haikuwa nuru bali giza isiyo na nuru.

Sam wa Sundi: Ukombozi wa kweli ni ule wa nafsi, pasi na kufuata kanuni na itikadi za watu wengine.

Lung'afa: Ukombozi usio na nta wala doa. Ukombozi wake si mwigo wala shauku iliyomo ya kujitaka kuchukua ushukani wa safari yake hapa duniani. Ukombozi huu ni wa kuzibia dunia masikio na kuifungulia macho.

Sam wa Sundi: Kabisa, kufumbua macho. Kutizama ukweli wa mambo na kuyaelewa jinzi yalivyo. Sio kufungua maskio na kuskiliza uvumi.

Lung'afa: Uvumi ni sanaa ya ibilisi kumpumbaza na kumshibisha yeyote aliye na kiu cha matamanio. Ikiwa utakubali kuiacha hata tunu ya mwanya ya sikio lako basi papara huyo atajaza na maneno matamu matamu hadi tunu ikawa Ua. Ua mwanangu, ua wa maua yenye miba! Ua usio na mpenyo wa wazo la busara.

Sam wa Sundi: Babu, kwa leo wacha nilaze nyama na damu. Kesho nitaendelea na safari ya kujikwamua kwa kasumba potovu.

Lung'afa: Pono ni muhimu. Ikiwa kiasi chake. Wingi wake ni sawa na uchache wake kwani kiwiliwili kina mahitaji yake. Jilaze pema, lalia ubavu usije ukamuka kilema kwani tushaalemea. Ndoto nazo usizisahau kwa maana ulalapo mbigu nayo huwa yawaza kukuhusu, nyota zikibadilishana nafasi. Inshallah.

Comments