Skip to main content

Featured

The struggle with many a rigid Logooli cultural practices

  The Logooli community is one of the deeply cultured societies – with near everything supposed to have been done as per custom – to allow another custom to follow. One example is that for a mature man (with a child or more) to be buried, there must be a house structure at home. Another is that a boy must be circumcised and nursed in father land. If maternal family decides to, the boy will have a hard time reconnecting with father people - a dent on his masculinity. There were two children who got burnt to death in a house in Nairobi. The single mother had left for night work. Elders were told that one of the children was Logooli. The other, the woman had sired with someone else. The Logooli family wanted to burry their little one and long discussed the do’s and don’ts. Of a man who died childless and the grave was placed as if he had died as a man with children. It should have been dug on the sides, the grave. A real thorn should have been thrust in his buttocks, his name go...

Fainali za mijadala ya shule za msingi - 2

Tumelianza juma la fainali za mashindano yetu ya mijadala. Ijumaa ya tarehe 26 mwezi huu wa Julai ndiyo siku shule nne zitapambana kwenye nusu fainali na kisha fainali ili maktaba ya Saniaga iliyopo Wangulu ipate mshindi wa Mijadala yake, huu ukiwa wa pili tangu tulipoanza kirasmi mashindano ya mijadala. 

Kama ilivyosemwa awali,  mijadala ya maktaba ya Saniaga ina nia ya kukuza na kuendeleza isimu kuu ya jamii kifikra na kivitendo. Wanafunzi na walimu wanahusishwa katika utafiti na uvumbuzi wa mienendo na hulka halisi, kuihaiisha katika maongezi na matumizi, kuieneza na kuikuza kwa minajili ya tuliopo na vizazi vijavyo. 

Kwa jinsi hii mijadala yetu ina mada pime kulingana na mafunzo yanayotokana na kujihusisha kwenye mashindano. Umbali huu tumeweza kuhusisha wanafunzi vilivyo na ni furaha yetu kwamba isimu asili yazidi kupata ufahamu miongoni mwao. 

Wanapokamilisha mada ya Nyimbo za Kale muhula huu wa pili (walivyokamilisha mada ya muhula wa kwanza iliyokuwa kwenye lugha ya kiingereza 'Use of mother tongue as a guiding and counseling tool in primary schools'), twatarajia kwamba mashindano ya mwaka ujao yatakua ya kufana zaidi yakiwa na mada nzito ili kuendelea kukuza isimu kuu yetu. 

Washindi watatuzwa, walimu na wanafunzi. Maktaba ya Saniaga na shirika lote la Saniaga litanufaika pia hivi kwamba malengo yake yanazidi kupata ufanisi na uhusikaji wa jamii ili iendelee katika ustawi wake. Kila mmoja wetu atakua wa furaha. 

Ni hapo basi mwakaribishwa nyote katika mashindano haya, mujionee jinsi wadogo watakao ridhi uzuri wetu (ubaya twauficha) wanavyoelezana kinagaubaga. Njooni mujifahamishe mengi kuhusu Maktaba ya Saniaga. Na muhimu njooni ili tunapotuza washindi na kuhimiza waliokosea kutia bidii wakati ujao, tuone ni vipi tutazidi kutia bidii kwenye malengo mengine ya shirika la kijamii la Saniaga. 

Mwaminifu, 

Comments